1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri wa ndani asema washukiwa ugaidi wauawe

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBia

Rais wa Ujerumani,Horst Köhler ametoa wito kwa waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble ajizuie zaidi anapotoa mapendekezo yake kuhusu njia za kupiga vita ugaidi.Köhler amesema, Schaüble kama mkuu wa wizara hiyo ana wajibu wa kutafuta njia zinazofaa,lakini mara nyingi, mapendekezo anayotoa kidogo kidogo,ni vigumu kukubaliwa na umma.Amesema,ana shaka zake ikiwa hatua ya kuwaua washukiwa ugaidi bila ya kufikishwa mahakamani,inaweza kuchukuliwa kwa urahisi hivyo.Waziri Schäuble wa chama cha kihafidhina cha CDU,amependekeza kuwa mtu anaeshukiwa ugaidi auliwe.Pendekezo hilo ni mtihani mkubwa kwa serikali ya mseto.Kiongozi wa kundi la SPD bungeni,Peter Struck amesema, Schäuble muda baada ya muda,anatoa sura ya kitisho na thamani ya kimsingi ya katiba inahatarishwa.