1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Waziri ataka wanaoshukiwa kufanya fujo wawekwe kizuizini.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3H

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble anafikiria kutumia hatua ya kuwaweka kizuizini watu wanaoonekana kuwa wanataka kufanya ghasia kabla ya mkutano wa mwezi ujao wa mataifa tajiri duniani G8 mjini Heiligendamm nchini Ujerumani.

Katika mahojiano kadha , Shäuble amesema kuwa watu wanaweza kuwekwa kizuizini hadi kwa wiki mbili iwapo kuna ushahidi mkubwa kuwa wanapanga kufanya ghasia katika mkutano huo.

Serikali inatarajia kiasi cha waandamanaji 100,000 kujikusanya katika mahali pa mkutano katika pwani ya bahari ya Baltic kwa ajili ya mkutano huo utakaoanza Juni 6-8.

Siku ya Jumatano , zaidi ya watu 5,000 waliandamana katika miji kadha ya Ujerumani dhidi ya msako uliofanywa na polisi ambao ulilenga maeneo 40 yanayotuhumiwa kuwa yanahusika na wanaharakati wa mrengo wa shoto.