1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Watu 68 wakamatwa mjini Berlin

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5Y

Polisi mjini Berlin wamewakamata watu 68 mapema leo kwenye machafuko ya sikukuu ya wafanyakazi.

Msemaji wa polisi mjini humo amesema watu waliwarushia chupa na mawe maofisa wa usalama lakini hakuwa na habari zozote kuhusu majeruhi.

Msemaji huyo amesema watu hao walikamatwa katika wilaya ya mashariki ya Friedichshain mjini Berlin wengi wao wakiwa vijana waliokuwa wamelewa.

Polisi mjini humo wanajiandaa kwa machafuko zaidi leo ikiwa ni sikukuu ya wafanyakazi inayoadhimishwa kwa maandamano na tafrija zinazohudhuriwa na maelfu ya watu mjini Berlin.

Mji mkuu Berlin umekuwa ukishuhudia machafuko kila tarehe mosi mwezi Mei tangu mwaka wa 1987. Katika miaka ya hivi karibuni motokaa za kifahari zilichomwa moto huku wapinzani wa serikali wakiwavurumishia mawe na chupa maafisa wa polisi.

Maafisa 5,000 wa polisi wametumwa kushika doria mjini Berlin hii leo katika juhudi za kuzuia machafuko mjini humo.