1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wasiwasi wa mgomo wa madereva wa treni wapungua

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBV5

Wasiwasi miongoni mwa abiria wa treni nchini Ujerumani sasa unaelekea kumalizika kufuatia makubaliano ya madereva wa treni kutofanya mgomo uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi ujao.

Duru zinasema wajumbe wa chama cha wafanyakazi wamekubalia kuendelea na mazungumzo na shirika la reli la hapa Ujerumani, Deutsche Bahn.

Mazungumzo hayo yalianza wiki mbili zilizopita katika juhudi ya kuutanzua mgogoro juu ya madai ya kutaka nyongeza za mishahara.

Shirika la reli la Ujerumani lilikabiliwa na migomo kadhaa mwanzoni mwa mwaka huu, lakini likafikia makubaliano na vyama viwili vya wafanyakazi wa reli ambao wanachama wao walikubali nyongeza ya mshahara kwa asilimia 4.5. Madereva wa treni waliyakataa makubaliano hayo.