1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Waraka wa pili wa amri ya kuuwa wapatikana

16 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYl

Waraka wa pili wenye kuonyesha amri ilioandikwa kwa maandishi na usalama wa taifa wa iliokuwa Ujerumani Mashariki wa kuwaua kwa kuwapiga risasi watu wanayoikimbia nchi hiyo ya kikomunisti imeripotiwa kuwa umepatikana kutoka kwenye nyaraka za siri za polisi zilizohifadhiwa.

Kugunduliwa kwa nyaraka hizo katika mji wa mashariki wa Chmenitz kumekuja baada ya waraka kama huo kuchapishwa mwishoni mwa juma na kupelekea uchunguzi kuangalia uwezekano wa kuanzisha mashtaka mapya ya uhalifu.Waraka wa kwanza ambao ulipatikana katika mji wa mashariki wa Magdeburg umeonyesha kwamba wizara ya usalama wa taifa inayojulikana kwa jina la Stasi iliwaagiza walinzi hapo mwaka 1973 kuwauwa kwa kuwapiga risai watu wanaotaka kukimbia Ujerumani Mashariki wakiwemo wanawake na watoto.

Idara ya nyaraka za Stasi imesema nakala ya pili ya amri hiyo tafauti na ile ya kwanza imesainiwa na kamanda mmoja.

Viongozi wa zamani wa Ujerumani Mashariki wameendelea kukanusha kwamba kulikuwepo na amri hizo.