1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wanaopanga mashambulizi ya kigaidi kufungwa miaka 10.

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOV

Waziri wa sheria wa Ujerumani Brigitte Zypries amewasilisha sheria mpya ambayo itasababisha kifungo cha hadi miaka 10 kwa wale watakaokuwa magaidi ambao wanahudhuria mafunzo katika kambi na kupanga mashambilizi, pamoja na wale wanaotoa fedha kwa ajili hiyo.

Zypries amesema muswada huo wa sheria pia utafanya kuwa rahisi kuwarudisha makwao raia wa kigeni ambao wanaonekana kuwa hatari. Hatua hiyo inafuatia kukamatwa kwa manaodaiwa kuwa magaidi wa Kiislamu nchini Ujerumani wiki mbili zilizopita.Wakati huo huo chama cha wanajeshi nchini Ujerumani kimetupilia mbali pendekezo la waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung kuwa ndege zilizotekwa nyara zitunguliwe ili kuepuka shambulio kama la Septemba 11.

Msemaji wa chama hicho Bernhard Gertz amewataka marubani wa ndege za kijeshi kukataa amri hizo, akisema kuwa zinakiuka sheria za msingi za Ujerumani. Bunge la Ujerumani linatarajiwa kujadili matamshi hayo ya Jung leo Jumatano.