1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Wanahistoria watachunguza mchango wa Wanazi katika wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani

12 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvL

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, amewateuwa wanahistoria watano kuuchunguza mchango wa zamani wa Wanazi katika wizara ya mambo ya kigeni. Jopo hilo litakuwa pamoja na wasomi wa Kimarekani na wa Ki-Israeli. Kazi yake itakuwa kuweka wazi juu ya mchango hasa wa wizara hiyo baina ya mwaka 1933, wakati Adolf Hitler, alipotwaa madaraka, na kushindwa Ujerumani vitani katika mwaka 1945. Wasomi hao watachunguza kwa kiwango gani wanadiplomasia wa wakati wa enzi za Wanazi walivoajiriwa tena na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.

Mwanzoni mwa mwaka huu, waziri Fischer alikomesha mtindo wa kutoa pongezi kwa wafanya kazi waliokufa katika gazeti la wafanya kazi wa wizara hiyo baada ya kutolewa pongezi kwa balozi mdogo wa zamani ambaye aliwahi kuwa muendeshaji mashtaka wakati wa enzi za wanazi.