1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Waliojaribu kumuua Hitler wakumbukwa nchini Ujerumani.

21 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEsW

Kumbukumbu zimefanyika nchini Ujerumani kuwakumbuka wahanga wa mauaji wa wanazi, wakati taifa hili likikumbuka juhudi zilizoshindwa dhidi ya maisha ya Adolf Hitler hapo Julai 20 1944.

Kundi la watu wakiongozwa na afisa wa jeshi Klaus von Stauffenberg walijaribu kumuua Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia kwa bomu lililowekwa katika makao yake makuu huko Prussia ya mashariki ya zamani.

Hitler alinusurika na shambulio hilo na watu waliohusika waliuwawa.

Katika sherehe ya kuweka mashada ya maua jana Jumatano katika jumba la makumbusho la Plötzensee mjini Berlin, waziri wa sheria wa Ujerumani Brigitte Zypries amesema kuwa licha ya kwamba mpango huo ulishindwa lakini ilikuwa ni juhudi za maana . Kiasi cha wapinzani wa kisiasa na wapiganaji waliokuwa wakimpinga Hitler kutoka mataifa 19 waliuwawa katika jela ya Plötzensee wakati wa enzi za utawala wa Wanazi.