BERLIN: Wajerumani kukabili ushindani wa Asia
20 Septemba 2005Rais wa Ujerumani bwana Horst Köhler amewataka wajerumani wajifunze na wakati huo huo waikabili changamoto ya ustawi wa haraka wa nchi za Asia.
Akifungua maadhimisho ya wiki ya nchi za Asia na Pasifik rais Köhler amesema mjini Berlin kwamba, wajerumani hawana budi watambue fursa na changamoto zinazotokana na ustawi wa bara la Asia.
Kiongozi huyo wa Ujerumani ameshauri kwamba nchi yake inaweza kujifunza kutoka kwa nchi za Asia.Rais Köhler amesema anaelewa wasiwasi wa watu nchini Ujerumani juu ya kupoteza nafasi zao za kazi kutokana na ushindani wa nchi za Asia lakini ameeleza kwamba haiwezekani kuepuka ushindani huo.
Hatahivyo bwana Köhler amesisitiza ulazima wa kuwapo haki katika mahusiano duniani.