BERLIN: Wajerumani kufanya kazi mpaka umri wa miaka 67
30 Novemba 2006Matangazo
Waziri wa kazi wa Ujerumani,Franz Münterfering ametetea uamuzi uliopitishwa na serikali kuhusu umri wa kustaafu wafanyakazi.Kuambatana na uamuzi huo,wafanyakazi watastaafu watakapofikia umri wa miaka 67.Hatua hiyo imepingwa vikali na upande wa upinzani na pia mashirika ya kijamii.Waziri Münterfering lakini amesema,watu wanazidi kuwa na umri mkubwa na kwa hivyo wanapokea malipo ya uzeeni kwa muda mrefu zaidi.Kwa hivyo kwa kupandisha umri wa kustaafu vizazi vya kesho vitasaidiwa.