BERLIN: Wajerumani 2 wametekwanyara Afghanistan
19 Julai 2007Matangazo
Serikali ya Ujerumani imethibitisha kuwa Wajerumani 2 waliotoweka nchini Afghanistan, huenda ikawa wametekwa nyara.Msemaji wa serikali ya Ujerumani mjini Berlin,alieleza kuwa watu hao wawili ni wahandisi katika kampuni moja nchini Afghanistan.
Kwa upande mwingine,polisi katika wilaya ya Vardak,katikati ya Afghanistan ilisema,Wajerumani hao 2 wametekwa nyara pamoja na dreva na mkalimani wao.Wizara ya ndani ya Afghanistan, mjini Kabul imesema,hatua za kuwasaka mahabusu hao zimeimarishwa.