BERLIN: Wajerumani 2 wametekwa nyara Afghanistan
19 Julai 2007Matangazo
Raia 2 wa Kijerumani wametekwa nyara nchini Afghanistan.Kwa mujibu wa polisi watu hao walikuwa wakifanyia kazi mradi wa kujenga bwawa katikati ya Afghanistan.Polisi imesema,hadi hivi sasa haikuwasiliana na wateka nyara wa Wajerumani hao wawili.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani,ubalozi wa Ujerumani katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul na wahusika wengine wanakusanya habari ili wajue zaidi kuhusu tukio hilo.