BERLIN: Wageni waendelea kuhamishwa kutoka Lebanon
20 Julai 2006Matangazo
Serikali nyingi za kigeni zinahimiza juhudi za kuwahamisha raia wake kutoka Lebanon.Ujerumani inafanya matayarisho makubwa kabisa ya kuwahamisha raia wake kutoka eneo hilo la mgogoro.Mabasi hamsini yamekodiwa kuwahamisha kiasi ya Wajerumani 3,000 waliyokusanyika mjini Beirut.Wajerumani hao watapelekwa Damascus,mji mkuu wa Syria na kutoka huko watarejeshwa nyumbani.Tangu Ijumaa iliyopita,zaidi ya Wajerumani 750 wamerejea nyumbani,wengi wao wakipitia Cyprus.Jeshi la majini la Marekani limepeleka meli tisa kusaidia kuwahamisha kiasi ya Wamarekani 2,400 kutoka Lebanon.Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema,hadi mwishoni mwa juma,kiasi ya Waingereza 5,000 watahamishwa kutoka eneo hilo la mapigano.