BERLIN: Vikosi vya Ujerumani kuendelea kushika doria katika pwani ya Lebanon
13 Septemba 2007Matangazo
Vikosi vya Ujerumani vitaendelea kushika doria katika pwani ya bahari ya Mediterenia iliyo himaya ya Lebanon kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.
Serikali ya Ujerumani mjini Berlin imerefusha muda wa wanajeshi hao kuendelea kubakia katika eneo hilo.
Hata hivyo idadi ya wanajeshi wa Ujeruamni katika pwani ya Lebanon itapunguzwa kwa karibu asilimia hamsini kutoka 2,400 hadi kufikia 1,400. Ujerumani inaongoza kikosi cha Umoja wa Mataifa, UNIFIL, kinachoilinda pwani ya Lebanon ili kuzuia uingizwaji silaha kinyume cha sheria kwa wanamgambo wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon.