BERLIN : Verdi yazungumza tena na Telekom juu ya mgomo
14 Juni 2007Matangazo
Chama cha wanafanyakazi nchini Ujerumani Verdi kimeanza tena mazungumzo na uongozi wa kampuni ya simu ya Telekom katika jaribio la kumaliza mgomo wa wiki tano.
Maelfu ya wafanyakazi wa Telekom wamekuwa kwenye mgomo tokea mwezi uliopita kutokana na mpango wa kampuni hiyo kupunguza gharama za wafanyakazi 50,000.Verdi inasema inatarajia kumaliza mgomo huo wa wafanyakazi katika siku chache zijazo.
Kampuni hiyo kubwa kabisa ya mawasiliano ya simu nchini Ujerumani inapanga kuanzisha vitengo vipya vyenye ushindani zaidi vya kuwahudumia wateja kwa wafanyakazi 50,000 ambao watafanya kazi kwa muda mrefu zaidi na kwa malipo kidogo.