Berlin. Ushahidi mpya wapatikana dhidi ya jeshi la Staasi.
13 Agosti 2007Nchini Ujerumani , waraka uliotangazwa mwishoni mwa juma umetoa ushahidi mpya wa amri ya maandishi kwa wanajeshi wa iliyokuwa Ujerumani ya mashariki DDR, kuwapiga risasi wale wanaotaka kutoroka kutoka nchini humo ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto , kwenda upande wa Ujerumani ya magharibi.
Waraka huo uliotolewa Oktoba mosi, 1973 na kupatikana wiki iliyopita katika ofisi ya nyaraka za zamani katika mji wa Magdenburg ulioko upande wa mashariki ya Ujerumani, unaonyesha kuwa wizara ya usalama wa taifa ambayo ilijulikana kama Staasi, iliwaamuru walinzi kuwa ni lazima wawazuwia ama kuwauwa, wale watakaojaribu kukimbilia upande wa magharibi.
Marianne Birthler, ambaye anaongoza idara inayoangalia ofisi hiyo ya askari kanzu wa Staasi, amesema waraka huo ni muhumu kwasababu viongozi wa kisiasa wa wakati huo wanaendelea kukana kuwa kulikuwa na amri hiyo ya kuuwa.