1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Umoja wa Ulaya washerehekea miaka 50

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFY

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameadhimisha miaka 50 tangu kuwekwa msingi wa Mkataba wa Rome kwa kuhudhuria tamasha ya muziki.Mkataba wa Rome ndio uliweka msingi wa Umoja wa Ulaya ambao sasa una wanachama 27.Kansela Angela Merkel wa Ujerumani aliwakaribisha viongozi wa dola na serikali wa nchi za Umoja wa Ulaya katika sherehe rasmi kwenye jengo la Berlin Philharmonica.Viongozi hao hii leo watatia saini waraka unaoitwa, ”Azimio la Berlin”.Waraka huo unabainisha maadili ya pamoja ya Umoja wa Ulaya na malengo yake katika siku zijazo.Katiba ya Ulaya ni mada mojawapo kuu ya Kansela Merkel wakati ambapo Ujerumani imeshika wadhifa wa urais unaozunguka kila miezi sita katika Umoja wa Ulaya.Merkel amesisitiza umuhimu wa kufanya mageuzi katika umoja huo ili kuweza kupambana na changamoto za siku zijazo.Rais wa Ujerumani,Horst Köhler vile vile ametoa wito wa kufanywa mageuzi katika Umoja wa Ulaya.