1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ukanda wa mateka wa Kijerumani ni wa zamani

11 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQh

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema kwamba ukanda wa video uliotolewa hivi karibuni wa mateka wa Ujerumani yumkini ukawa ni wa zamani kuliko vile inavyoaminika.

Msemaji wa wizara hiyo amesema ukanda huo wa video ulikuwa tayari kwenye mtandao kabla ya kujulikana kwake.Kwenye ukanda huo kundi la waasi nchini Iraq limetishia kumuuwa mateka huyo wa Kijerumani iwapo serikali ya Ujerumani haitowaondowa wanajeshi wake kutoka Afghanistan katika kipindi cha siku 10.

Ukanda huo wa video umemuonyesha Sinan Krause akiwa na mama yake Hannelore.Wote wawili walitekwa na kundi hilo la waasi linalojiita Kikosi cha Mishale ya Haki mwanzoni mwa mwaka huu.

Waasi hao wa itikadi kali walimwachilia huru mama huyo hapo mwezi wa Julai wakati walipodai kwamba alibadili dini kuwa Muislamu.