BERLIN: Ujerumani yatoa wito wa amani Ukraine.
26 Mei 2007Matangazo
Ujerumani imeungana na Russia kuwatahadharisha viongozi wa Ukraine dhidi ya kutumia nguvu kutatua mzozo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo.
Afisa wa kibalozi wa Ujerumani, Johannes Regenbrecht amesema kwenye mkutano na Waziri Mkuu Viktor Yanukovych kwamba mzozo uliopo wa kuwania mamlaka kati ya waziri mkuu huyo na Rais Viktor Yuschenko unapaswa kudhibitiwa ili usisababishe ghasia zaidi kwani hali hiyo itaathiri uhusiano kati ya Ukraine na Ulaya.
Mzozo kati ya viongozi hao wawili ulifikia upeo jana wakati rais huyo alipoanza kudhibiti vikosi vya usalama wa ndani ambavyo kwa kawaida husimamiwa na waziri wa mambo ya ndani.