1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yasema kampuni ya Airbus itaamua kuhusu ajira

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQ9

Serikali ya Ujerumani imesema kampuni ya ndege ya Airbus, itaamua kuhusu kupunguza nafasi za ajira.

Akitofautiana na matamshi ya waziri mkuu wa Ufaransa, Dominique de Villepin, kwamba mpango wa kuiunda upya kampuni hiyo utasababisha nafasi elfu 10 za ajira kupotea, msemaji wa serikali ya Ujerumani ameifutilia mbali idadi hiyo akisema ni tetesi tu.

Msemaji huyo amekanusha kwamba swala hilo litaamuliwa Ijumaa wiki hii wakati wa mkutano baina ya kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel na rais Jacques Chirac wa Ufaransa. Amesema kuiunda upya kampuni ya Airbus ni jukumu la viongozi wa kampuni hiyo.

Angela Merkel na Jacque Chirac wanatarajiwa kukutana Ijumaa ijayo karibu na mji mkuu Berlin kama sehemu ya mpango wa mikutano yao ya kila mara baina ya Ujerumani na Ufaransa.