1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani yaipatia Somaliland msaada wa euro 455,000.00

19 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLg

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani chini ya mpango wa msaada wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limetowa msaada wa euro 455,000.00 kwa Jamhuri ya Somaliland ili fedha hizo zitumike kwenye mradi wa kuteguwa mabomu yaliotegwa ardhini.

Fedha hizo zinatazamiwa kutumika kufunza kikosi maalum cha askari polisi kwa ajili ya shughuli hiyo pamoja na kuteguwa mabomu yaliotegwa kaskazini mwa Jamhuri ya Somaliland.

Jamhuri ya Somaliland imekuwa na ushirikiano na Umoja wa Ulaya tokea mwaka 1998 hadi mwaka 2002.Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani hadi sasa imegharamia euro milioni 2. 3 kwa shughuli hiyo.