1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yachunguza madai ya kutekwa nyara raia wake mwengine Afghanistan

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfQ

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ujerumani imesema inachunguza ripoti ya kutekwa nyara mwandishi wa habari mjerumani pamoja na mkalimani wake raia wa Afghanistan.

Msemaji wa wizara hiyo mjini Berlin amesema ubalozi wa Ujerumani mjini Kabul unafanya kila inaloweza kutafuta ukweli kuhusiana na taarifa hiyo.

Maafisa wa jimbo la Kunar mashariki mwa Afghanistan wametangaza kutekwa kwa mwandishi huyo wa habari pamoja na mkalimani wake wakati walipokuwa wakijaribu kukifikia kijiji ambako raia 23 waliuwawa kwenye shambulio la angani lililofanywa na majeshi ya jumuiya ya NATO majuma kadhaa yaliyopita.

Mwandishi huyo wa habari na mkalimani wake walitekwa nyara katika wilaya ya Saangar mkoani Kunar wakiwa ndani ya nyumba.

Sambamba na hayo kundi la Taliban limetishia kuwaua baadhi ya mateka wa Korea Kusini kufikia leo saa nane ikiwa serikali ya Afghanistan hitawaachia huru wafungwa wa Taliban.