BERLIN: Ujerumani kutoa mafunzo kwa walimu wa kijeshi
10 Mei 2007Matangazo
Serikali ya Ujerumani ipo tayari mwaka huu kutoa mafunzo kwa walimu 350 wa jeshi la Iraq na kuvipatia vikosi vya Kiiraqi magari 150 ya kawaida.Tangazo hilo limetolewa na waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung baada ya kukutana na waziri mwenzake wa Irak,Abdul Qadir Obeidi mjini Berlin.Jeshi la Ujerumani limeshatoa mafunzo kwa walimu wa kijeshi wapatao 450 katika miradi mbali mbali.Mafunzo hayo yametolewa katika vituo viliopo Umoja wa Falme za Kiarabu na huku Ujerumani pia.