1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani kushiriki katika jeshi la kulinda amani Lebanon

17 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDL6

Serikali ya Ujerumani imesema kimsingi imekubali kutoa mchango wa askari watakaoshiriki katika jeshi la kimataifa la kulinda amani nchini Lebanon.

Lakini Ujerumani inastahabu kulinda pwani za Lebanon pamoja na kuweka askari kwenye mpaka baina ya nchi hiyo na Syria.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani bwana Franz Joseph Jung leo anatarajiwa kuwasilisha pendekezo juu ya jinsi nchi yake itakavyoshiriki katika jeshi hilo la kimataifa.