1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani kuisaidia Lebanon

6 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSM

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameahidi kusaidia kuijenga upya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr al Bared nchini Lebanon baada ya wanajeshi wa Lebanon kuiteka kutoka kwa wanamgambo wa Kiislam wiki iliopita.

Merkel pia amesema Ujerumani itaisaidia Lebanon kuimarisha asasi zake za demokrasia hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika nchini humo mwishoni mwa mwezi wa Septemba.Angela Merkel na mawaziri wengine wa Ujerumani wamekuwa wakikutana na Waziri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora mjini Berlin.

Siniora amesema ni muhimu kuijenga upya kambi hiyo na kuwa chini ya mamlaka ya taifa la Lebanon kwa kuwa hili ni jambo ambalo mtu anaweza kujifunza kutokana na uzoefu na kwamba serikali ya Ujerumani itaendelea kuisaidia Lebanon.

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani ameahidi kutowa euro nyengine za ziada milioni mbili kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina walioko nchini Lebanon.