BERLIN: Ujerumani kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Uganda
16 Juni 2007Matangazo
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekutana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda mjini Berlin.Baada ya mazungumzo yao,Merkel alisema,atachukua hatua za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Uganda. Akaongezea kuwa ni muhimu kwamba Uganda iliyokuwa nchi yenye kilimo,imefanikiwa kuwa taifa lenye viwanda.Kwa upande wake,Rais Museveni alisema, angependa kuona msaada zaidi wa Ujerumani katika sekta za elimu,miundo mbinu na njia za kuwa na matumizi bora ya nishati.Akaongezea kuwa Uganda inahitaji msaada wa kibiashara,kwa sababu nchi hiyo inatazamia kutengeneza na kuuza bidhaa zake ili ipate kuwa jumuiya ya kisasa.