BERLIN: Ujerumani kuendelea na ujumbe wa Afghanistan
17 Agosti 2007Matangazo
Wanasiasa katika mji mkuu wa Ujerumani,Berlin wamesisitiza kuwa Ujerumani inapaswa kuendelea na jukumu la kulinda usalama na kusaidia kuijenga upya Afghanistan,licha ya kuuawa kwa polisi watatu wa kijeshi wa Ujerumani.
Wajerumani hao watatu waliuawa siku ya Jumatano, nje ya mji mkuu wa Afghanistan,Kabul baada ya gari lao kulengwa na bomu lililoripuliwa kutoka kwa mbali.Wataliban wamesema,wao ndio waliofanya shambulizi hilo.Wapelelezi wa Kijerumani wapo Kabul kuchunguza mauaji hayo.