1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani itaimarisha msaada Afghanistan

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AA

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel baada ya kurejea kutoka ziara yake fupi ya ghafula nchini Afghanistan amesisitiza kuwa wanajeshi wa Kijerumani hawatopelekwa kubakia katika eneo la mapigano kusini mwa Afghanistan.Amesema, ikihitajika,msaada utatolewa kwa majeshi ya madola shirika yalio kusini mwa Afghanistan.

Kansela Merkel alipokutana na Rais wa Afghanistan Hamid Karzai mjini Kabul,alimuhakikishia kuwa Ujerumani itaimarisha msaada wa kutoa mafunzo kwa polisi.Amesema,Afghanistan inapaswa kusaidiwa ili iweze kudhamini usalama wa nchi,hatua kwa hatua. Kabla ya kurejea Ujerumani,Kansela Merkel alikwenda Mazar-i-Sharif kambi kuu ya vikosi vya Ujerumani,iliyo kaskazini mwa Afghanistan.Ziara ya Merkel nchini Afghanistan iliwekwa siri mpaka dakika ya mwisho kwa sababu za usalama.