1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani ina matumaini na mkutano kwa ajili ya mashariki ya kati.

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1I

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameeleza matumaini yake makubwa kwa mkutano ujao wa kimataifa kuhusu mashariki ya kati nchini Marekani. Akizungumza mjini Berlin, baada ya mkutano na mfalme Abdullah wa Jordan, Merkel amesema anamatumaini mazungumzo hayo yatakuwa hatua ya kwanza kuelekea katika suluhisho la kudumu katika mzozo wa mashariki ya kati. Amesema kuwa Ujerumani inataraji kuchukua nafasi ya juu katika hatua za amani. Mfalme Abdullah amesema kuwa anazikaribisha juhudi za Ujerumani na anamatumaini mkutano huo wa kimataifa utasaidia kusafisha njia kuelekea makubaliano ya amani katika mashariki ya kati.