1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani hatarini kushambuliwa na magaidi

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIs

Gazeti la Financial Times Deutschland limesema polisi wa shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani BKA wameonya kwamba hatari juu ya uwezekano wa magaidi kushambulia Ujerumani iko katika kiwango cha juu kabisa kuwahi kushuhudiwa kwa mingi mingi.

Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imekataa kuzungumzia juu ya repoti hiyo.Jumamosi iliopita kundi lisilojulikana sana la waasi nchini Iraq limetisihia kwenye ukanda wa video kuwauwa Wajerumani waliowateka nyara mjini Baghad venginevyo Ujerumani inaondowa wanajeshi wake walioko nchini Afghanistan.

Hapo jana Rais Horst Köhler wa Ujerumani amewasihi hadharani wateka nyara hao kuwaachilia Wajerumani hao mama mtu na mwanawe wa kiume.

Rais Köhler wa Ujerumani ametowa wito huo katika ujumbe ulioko kwenye ukanda wa video uliotangazwa nchini Ujerumani na katika mataifa ya Kiarabu.