BERLIN: Uchumi wa Ujerumani unatarajiwa kukua kwa kiwango kikubwa mwaka huu
7 Aprili 2007Matangazo
Serikali ya Ujerumani inahakika kukua kwa uchumi wake kutaimarika zaidi mwaka huu kama ilivyotarajiwa hapo awali.
Waziri wa uchumi wa Ujerumani, Michael Glos, ameliambia gazeti la Bild am Sonntag kwamba kiwango cha asilimia 1,7 cha ukuaji wa uchumi kilichowekwa hapo awali, huenda kikaongezwa.
Waziri Glos amesema kunawiri kwa uchumi huenda kukalinufaisha soko la ajira huku idadi ya watu wasio na ajira ikishuka chini ya idadi ya watu milioni 3.5 wakati wa msimu wa machipuko.
Watu wasio na ajira nchini Ujerumani ni zaidi ya milioni nne.