BERLIN: Steinmeir aonya kuhusu mzozo wa katiba ya Ulaya
18 Juni 2007Matangazo
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, ameonya kwamba mzozo kuhusu kuifufua katiba ya Umoja wa Ulaya huenda uukwamishe mkutano wa umoja huo utakaofanyika mjini Brussels Ubelgiji wiki hii.
Baada ya kikao maalumu cha mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya mjini Luxembourg hapo jana, waziri Steinmeier alisema hakuna uhakika ikiwa mkutano wa mjini Brussels utafaulu.
Poland imetishia kutumia kura yake ya turufu kuitilia guu katiba ya Ulaya ikiwa mabadiliko hayatafanywa kwa mfumo wa kupiga kura uliopendekezwa kwenye katiba hiyo.