BERLIN: Steinmeir aitaka Marekani itizame upya mpango wake
22 Machi 2007Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir ameitaka Marekani kufikiria upya mpango wake wa kuweka makombora huko Poland na Jamuhuri ya Czech na kwamba umeiudhi Urusi.
Steinmeir amesema kuwa mpango huo wa Marekani unahatarisha kuigawa Ulaya, na kwamba badala yake Marekani ijenge imani kwa Urusi kwa kuwa na mazungumzo ya wazi juu ya mpango wake huo.
Marekani imepanga kuweka makombora hayo ya kujihami ikisema ni dhidi ya mataifa kama vile Iran.
Akiwa mjini Warsaw Poland, Waziri mdogo wa nje wa Marekani, Daniel Frid alisema kuwa makombora hayo yatailinda si Marekani peke yake bali pia Ulaya.