BERLIN: Steinmeier afanya ziara ya ghafula Urusi
15 Mei 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier hii leo anakwenda Moscow kwa ziara ya ghafula.Ziara hiyo inafanywa siku chache kabla ya kufanywa mkutano kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya uliokumbwa na mvutano na migogoro kati ya Urusi na baadhi ya wanachama wa umoja huo.Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya, atauongoza ujumbe wa umoja huo kwenye mkutano wa siku ya Ijumaa pamoja na Rais Vladimir Putin katika mji wa Samara nchini Urusi.