BERLIN: "Siku ya kuacha wazi Mlango"
25 Agosti 2007Matangazo
Katika mji mkuu wa Ujerumani,Berlin ofisi ya Kansela na jumla ya wizara 14 zipo wazi kwa umma kuanzia hii leo hadi Jumapili jioni.Siku hii ikijulikana kama „Siku ya kuacha mlango Wazi“ inaupa umma nafasi ya kutembelea ofisi za serikali.Huu ni mwaka wa tisa kwa serikali kukaribisha umma katika ofisi zake.Mwaka uliopita kiasi ya watu 155,000 waliitumia fursa hiyo kutembelea ofisi za Kansela na mawaziri wake mjini Berlin.