BERLIN: Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limekumbusha juu ya hali...
26 Novemba 2003Matangazo
mbaya za mayatima wa ukimwi barani Afrika, na wanahitaji msaada wa haraka. Idadi ya mayatima waliondokewa na wazazi wao kwa sababu ya ukimwi, hivi leo ni millioni 11, na idadi itapanda marudufu kukaribia millioni 20 ufikapo mwaka 2010, - alisema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa mwenye kuhusika na Ukimwi barani Afrika, Joseph Lewis, mjini Berlin. Kutokana na siku ya Ukumbusho wa Ukimwi Duniani, Jumatatu ijayo, aliwasilisha ripoti ya shirika la UNICEF juu ya hali za mayatima wa ukimwi barani Afrika.