1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Sherehe za miaka 50 ya mkataba wa Roma zaendelea Berlin.

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFR

Sherehe zinaendelea katika mji mkuu wa Ujerumani –Berlin, kuadhimisha miaka 50 tangu kusainiwa mkataba wa Roma uliokua chimbuko la hatimae kuundwa kwa Umoja wa ulaya. Kubwa katika sherehe hiyo litakua ni kusainiwa kwa “Azimio la Berlin”, na viongozi wa taifa na serikali wa umoja wa ulaya,ikiwa ni taarifa juu ya maadili ya pamoja ya umoja huo na malengo ya siku zijazo. Waraka huo hautarajiwi kuashiria moja kwa moja juu ya kizingiti kilipo juu ya kukwama kwa suala la kuidhinishwa katiba ya umoja huo. Mwenyekiti wa sasa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,aliipa kipa umbele mada ya kufufuliwa suala la katiba kuwa miongoni mwa masuala makuu katika kipindi hiki cha Ujerumani kama mwenyekiti wa umoja wa Ulaya-wadhifa unaozunguka miongoni mjwa nchi wanachama kila baada ya miezi 6.