1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Schroeder ziarani Afrika wiki moja

19 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhq
Kansela wa Ujerumani Gerhard SCHROEDER amewasili Ethiopia ikiwa ni hatua ya kwanza ya duru ya wiki moja katika Afrika na ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi tangu ashike madaraka mwaka 1998. Mjini Addis Ababa, Bwana SCHROEDER atahutubia mkutano wa Umoja wa Afrika kabla ya mazungumzo na Waziri Mkuu Meles ZENAWI wa Ethiopia. Baada ya Ethiopia, Kansela huyo wa Ujerumani atakwenda pia Kenya, Afrika Kusini na Ghana. Maafisa wa serikali ya Berlin wametaja kuwa ziara hiyo itakuwa fursa kwa Bwana SCHROEDER, anayeongoza ujumbe wa watu 23, wakiwemo wafanyabiashara, kuomba Waafrika kuleta mageuzi yanayohimiza ufumbuzi wa mizozo ya bara hilo.