1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Schroeder na Chirac washughulikia tatizo la katiba mpya

4 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF75

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amemualika rais Jacques Chirac wa Ufaransa kwa mkutano mjini Berlin.Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia mzozo uliozuka kuhusu katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.Watakapokutana kwenye chakula cha usiku baadae hii leo,viongozi hao wawili watajaribu kutafuta njia ya kusalimisha mkataba uliokataliwa na wapiga kura nchini Ufaransa na Uholanzi. Katika kura ya maoni iliyopigwa hivi karibuni,wapigaji kura katika nchi hizo mbili wameipinga katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.Siku ya Ijumaa Schroeder alishauri kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya wachukuwe wakati wa kuufikiria mkataba huo watakapokutana kati kati ya mwezi huu.Ujerumani na nchi zingine tisa za Ulaya zimeidhinisha katiba hiyo mpya,lakini wananchi wake hawakupewa nafasi ya kupiga kura ya maoni.Katiba hiyo mpya inahitaji kuidhinishwa na wanachama wote 25 katika Umoja wa Ulaya kabla ya kuweza kuingia kazini.Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa idadi ya wapinzani wa katiba hiyo inaongezeka nchini Denmark na Jamhuri ya Czech.Nchini Uingereza nako vyombo vya habari vinasema kuwa upigaji wa kura ya maoni nchini humo huenda ikaahirishwa.