1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Schroeder ayataka mataifa tajiri kusaidia zaidi mataifa masikini

28 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9W

.

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ameyataka mataifa yenye viwanda kujitahidi zaidi kuyasaidia mataifa yanayoendelea duniani.

Amesema kuwa atalipeleka suala hilo katika mkutano wa mataifa yenye utajiri wa viwanda G8 utakaofanyika nchini Scotland mwezi Julai.

Ametoa taarifa hiyo katika majadiliano yaliyofanyika katika siku ya pili ya mkutano wa kila mwaka wa makanisa ya Kiprotestant mjini Hannover.

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel raia wa Kenya Bibi Wangari Maathai amewaambia washiriki wa mkutano huo kuwa masuala ya ulinzi wa mazingira na demokrasia yanakwenda sambamba. Amesema kuwa mali chache zilizoko hapa duniani lazima zigawanywe kwa utaratibu wa haki, ili kuepuka matatizo. Mkutano huo wa kanisa la Waprotestant unaendelea hadi Jumapili.