1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Schröder atetea bajeti ya umoja wa ulaya

14 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3d

Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amewataka viongozi wa Umoja wa Ulaya kushirikiana pamoja katika kuiunda bajeti ya umoja huo ambayo itakubalika na nchi zote wanachama.

Uingereza hadi kufikia sasa bado imekataa kubadilishwa kwa mapatano ya mwaka 1984 juu ya kuiwezesha nchi hiyo kupunguziwa kutoa mchango wa thamani ya Euro billioni 4.6 kila mwaka.

Ufaransa na Ujerumani pia zimepinga kwa Uingereza kulipwa ruzuku za umoja wa ulaya zinazotolewa kwa wakulima.

Maswala haya ndio yatakayo pewa kipaumbele katika mkutano utakaofanyika hii leo mjini Paris kati ya waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair na rais Jacque Chiraq wa Ufaransa.

Viongozi wa umoja wa Ulaya watafanya mkutano wa dharura huko Brussels, Ubelgiji alhamisi ijayo kuzungumzia makisio ya bajeti ya kipindi cha mwaka wa 2007 hadi 2013.