1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Russia na Estonia zatakiwa kuwa na uvumilivu.

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC63

Umoja wa Ulaya umeitaka Russia na Estonia kuweka mbele uvumilivu katika mzozo wao kuhusiana na kuondolewa kwa kumbukumbu za kivita za wakati wa enzi za Urusi ya zamani katika mji mkuu wa Estonia, Tallinn.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, nchi ambayo inashikilia urais wa umoja wa Ulaya hivi sasa , amemtaka waziri mkuu wa Estonia Andrus Ansip na rais wa Russia Vladimir Putin kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja ili kutanzua mzozo huo.

Mtu mmoja ameuwawa na wengine 100 wamejeruhiwa katika ghasia ambazo zimezuka kufuatia kuondolewa kwa sanamu la mwanajeshi wa jeshi la Urusi ya zamani. Watu 600 wamekamatwa. Russia inawashutumu maafisa wa Estonia kwa kutumia nguvu kupita kiasi kuzima ghasia hizo.