1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Rubani afariki katika ajali.

13 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAR

Rubani mmoja amefariki dunia katika ajali ya ndege ya kijeshi ya Ujerumani nchini Uswisi. Maafisa wa nchi hiyo wamesema kuwa rubani mwingine amenusurika akiwa na majeraha machache.

Ndege hiyo ya kijeshi chapa Tonado ilikuwa ikirejea nchini Ujerumani kutoka katika safari ya kawaida ya mazoezi katika eneo la Corsica wakati ilipoanguka katika milima ya Alpine. Ujerumani ilituma hivi karibuni ndege sita chapa Tonado nchini Afghanistan wiki iliyopita kulisaidia jeshi la NATO katika operesheni za upelelezi ambapo jeshi hilo linapambana na wapiganaji wa Taliban.