1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Rais Chirac katika ziara ya kuaga

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC53

Rais Jaques Chirac wa Ufaransa amefanya ziara ya kuaga mjini Berlin kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini Ufaransa kumchaguwa mrithi wake hapo Jumapili.

Chirac amemwambia Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kwamba Ufaransa na Ujerumani lazima ziongoze katika kukamilisha katiba ya Umoja wa Ulaya na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Chirac ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 12 amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa wa kigeni kulihutubia bunge la Ujerumani ilioungana upya.Ametumikia kipindi chake kwa kuwa sambamba na Makansela watatu wa Ujerumani kwanza akiwa ni Helmut Kohl baadae Gerhard Schroeder na sasa Merkel.