Berlin. Rais aomba raia wake kuchiliwa huru.
15 Machi 2007Matangazo
Rais wa Ujerumani ametoa ombi la kuachiliwa mara moja kwa raia wawili wa ujerumani waliokamatwa nchini Iraq.
Horst Köhler ametoa wito huo katika ujumbe uliowekwa katika video ambao umetangazwa katika Ujerumani na mataifa ya kiarabu.
Jumamosi iliyopita , kundi la wapiganaji ambalo halikujulikana hapo kabla lilitishia katika ujumbe katika video kuwauwa watu hao wawili iwapo Ujerumani haitaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan katika muda wa siku kumi.