BERLIN: Raia wa kigeni wahamishwa kutoka Lebanon
19 Julai 2006Matangazo
Kiasi ya Wajerumani 300 wamesharejeshwa Ujerumani kutoka Lebanon na serikali mjini Berlin imesema inatazamia kuwahamisha raia wake wote kutoka Lebanon katika siku chache zijazo.Msafara mwingine wa mabasi utaondoka leo hii kuelekea Syria.Siku ya Ijumaa kutafanywa misafara zaidi ya ndege kuwarejesha nyumbani kiasi ya Wajerumani 400 kutoka mji mkuu wa Syria,Damascus.Serikali za nchi mbali mbali zinapeleka helikopta na meli kuhamisha maelfu ya wageni.Umoja wa Mataifa vile vile unawaondosha wafanyakazi wake wote wasio na kazi za dharura kutoka Lebanon.