BERLIN; Programu ya uchaguzi ya chama cha SPD Ujerumani
5 Julai 2005Kansela wa Ujerumani bwana Gerhard Schröder na mwenyekiti wa chama kinachotawala SPD bwana Franz Münterfering leo wametangaza programu ya uchaguzi ya chama chao.
Katika programu hiyo, chama cha SPD kinalenga shabaha ya kuzifanya hali za familia kuwa bora,kuimarisha bima za afya na kuhakikisha kwamba watu matabaka yote wanalipia bima hizo ikiwa pamoja na wanasiasa na watumishi wa serikali.
Kansela Schröder ameitathmini programu hiyo kuwa ushuhuda wa uwezo wa chama chake katika kutekeleza majukumu ya kisiasa. Amesema kwamba chama chake ndicho chenye uwezo wa kuleta maguezi nchini Ujerumani.
Kwa mujibu wa programu hiyo ,Ikiwa chama cha SPD kitashinda katika uchaguzi ujao,watu wanaopata mishahara mikubwa watatozwa kodi asilimia tatu zaidi .
.