1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Pande tatu kushirikiana katika maswala ya usalama

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCX

Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi zimekubaliana kushirikiana katika maswala ya usalama.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amesema malengo kadhaa yameafikiwa katika mkutano na mawaziri wenzake kutoka Washington na Moscow uliofanyika mjini Berlin.

Malengo hayo ya kiusalama ni pamoja na kushirikiana katika kupambana dhidi ya usajili wa vijana katika makundi ya kigaidi na pia vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya nchini Afghanistan.

Mawaziri hao wa mambo ya ndani pia wamekubaliana juu ya nia ya kuimarisha idara ya polisi ya kimataifa ya Interpol katika kupamabana na wizi wa stakabadhi za kusafiria.

Ujerumani imefadhili mkutano huo ikiwa ndio mwenyekiti wa nchi za umoja wa ulaya kwa sasa.