BERLIN : Oettinger asikitikia shutuma za wasifu
15 Aprili 2007Matangazo
Kufuatia kulaumiwa vikali na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani waziri mkuu wa jimbo la kusini la Baden-Wüttemberg ameelezea masikitiko yake kwa kile alichokiita kuwa kutofahamiana.
Günther Oettinger alimsifu sana waziri mkuu wa zamani wa jimbo hilo Hans Filbinger kuwa kama mpinzani wa utawala wa Manazi juu ya kwamba kwa kweli Filbinger alikuwa hakimu ya kijeshi katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ambaye aliwahukumu adhabu ya kifo Wajerumani waliolitoroka jeshi.
Oettinger amezikataa shutuma kwamba kwa njia fulani aidha alikuwa akihalalisha uhalifu wa Manazi.