Berlin. Nigeria kualikwa katika mkutano wa G8.
21 Mei 2007Matangazo
Ujerumani inatarajia kuwa , rais mteule wa Nigeria Umaru Yar’Dua atahudhuria mkutano wa mwezi Juni wa kundi la mataifa tajiri yenye viwanda G8 licha ya jumuiya ya kimataifa kutoridhika na uchaguzi uliompatia madaraka.
Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema kuwa inaendelea na utamaduni wa kuialika Nigeria , miongoni mwa mataifa mengine ya Afrika katika mkutano huo utakaoanza Juni 6-8.
Mataifa mengine ya Afrika yatakayowakilishwa katika mkutano huo katika mji wa pwani ya baltic nchini Ujerumani wa Heiligendamm ni pamoja na Misr, Algeria , Senegal, Afrika kusini na Ghana.
Kuhudhuria kwa Yar’Adua kutampa hata hivyo stahili kimataifa na pia nchini mwake.